Uchumi yafunga maduka yake TZ na UG

Maduka ya jumla ya Uchumi yametangaza kufungwa kwa oparesheni zake nchini Tanzania na Uganda katika zoezi la kubana matumizi .

151013171634_uchumi_640x360_bbc_nocredit

Mkurugenzi mkuu wa maduka hayo Dr.Julius Kipng’etich amesema kuwa bodi yake imeamua kufunga vituo hivyo kwa lengo la kutathmini muundo wa oparesheni zake nchini Kenya. ”Maduka yetu nchini Tanzania na Uganda yanajumlisha asilimia 4.75 ya oparesheni zetu licha ya kutugharimu asilimia 25 ya oparesheni zetu”.

Maduka ya uchumi katika mataifa hayo mawili hayajazalisha faida yoyote katika kipindi cha miaka 5 swala ambalo linalazimu faida zinazopatikana katika maduka ya Kenya kutumika,alisema Kipng’etich.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa tayari maduka hayo yameandika barua kwa Mamlaka ya masoko nchini Kenya ,soko la hisa pamoja na washikadau muhimu kuhusu uamuzi huo na kuongezea kwamba hivi karibuni uchumi itahitaji kuungwa mkono na wamiliki wa hisa ili kuidhinisha mpango huo.

Maduka yote katika mataifa hayo mawili yamefungwa.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s