Kampeni Zambadilisha Akili Johari

BLANDINA Chagula maarufu kama Johari, ambaye ni mmoja wa wasanii wanaozunguka nchi nzima kuipigia kampeni CCM katika uchaguzi mkuu, amesema baada ya kutembea na kufanya kazi, amejikuta akiihamishia akili yake katika siasa.

JOHARI466

“Kuna wakati nilikuwa naafikiana na yale madai kuwa serikali haijafanya lolote, lakini baada ya kuzunguka katika mikoa mbalimbali, nimejionea maendeleo yaliyopo na nimejifunza mambo mengi, nimepata hamasa kubwa ya kuingia kwenye siasa na huenda nikagombea ubunge uchaguzi ujao,” alisema muigizaji huyo wa siku nyingi.

Aidha, alisema alipokuwa Dar alizoea kuamka wakati wowote aliotaka, lakini ratiba za hivi sasa zimemfanya kuwa fiti zaidi kwa sababu ni kazi tu kuanzia asubuhi hadi jioni wakipita nyumba hadi nyumba, mtaa hadi mtaa jambo lililomfanya kubadilika kwa mambo yake mengi.

Chanzo:GP

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s