Makaidi wa NLD afariki dunia

Mwenyekiti wa chama cha NLD Dkt Emmanuel Makaidi ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Masasi na mwenyekiti mwenza wa UKAWA, amefariki dunia mchana wa leo mkoani Mtwara kwa shinikizo la damu.

Pix-10

Mke wa Mzee Makaidi Mama Modesta Makaidi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, ambapo amesema kuwa Makaidi amefariki leo majira ya saa 6 mchana katika hospitali ya mwambao iliyoko Wilayani Masasi mkoani Mtwara.

“Juzi tukiwa katika harakati za kampeni, alidai anajiskia vibaya, tukampeleka Zahanati, wakamcheki presha wakasema presha imepanda, lakini alipata matibabu akawa na unafuu, lakini leo asubuhi hali ikawa mbaya ndipo tukampeleka Mwambao Hospital, lakini ilipofika majira kati ya saa 5 na saa 6 akafariki” alisema mama Modesta.

Kuhusu taratibu za mazishi Mke wa marehemu Modesta Makaidi amesema kuwa taarifa zitatolewa baadaye lakini kuna uwezekano mkubwa wa mwili wake kupelekwa jijini Dar es salaam.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s