Rose Ndauka ajitosa kwenye muziki rasmi

Msanii maarufu wa Bongo Movie Rose Ndauka ameamua kujitosa kwenye muziki wa Bongo Flava na kuanzisha kundi la vijana wenye vipaji litakalosimamiwa na kampuni yake ya Rosie.

Rose-Ndauka

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio amesema vijana hao wametunga wimbo wa kuhamasisha amani katika kipindi hiki cha uchaguzi, ikiwa ni moja ya mchango wake kama msanii katika kufikisha ujumbe kwa wananchi.

“Hiki ni kipindi cha uchaguzi, kwa hiyo nikasema nitashiriki vipi mimi kama msanii kuwaelimisha Watanzania wenzangu ili tuwe na amani yani tuwe sawa, kwa sababu inaoneka hichi kipindi kumekuwa na machafuko, kwa hiyo nikataka na mimi kushiriki kwa namna moja au nyingine, nikasema njia pekee ambayo mimi naweza kushiriki nikawambiavijana wangu tungeni nyimbo ambayo inahamasisha amani Tanzania kwa kipindi hiki cha uchaguzi tukaingia studio”, alisema Rose Ndauka.

Rose Ndauka ameendelea kwa kusema kwamba pamoja na hayo kundi hilo litaendelea kutoa kazi hata baada ya uchaguzi, na pia licha kufanya muziki, pia wanaigiza na wana vipaji mbali mbli.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s