Tuzo haioneshi msanii amepiga hatua- Peter Msechu

Msanii Peter Msechu amesema kitendo cha kupata tuzo kwa msanii si kitendo cha kumuonyesha msanii huyo ndio amepiga hatua, bali inazidi kumtangaza baada ya kupiga hatua.

Msechu

Msechu ameyaongea hayo kweny Planet Bongo ya East africa Radio, na kueleza kwamba mpaka msanii kufikia hatua ya kuwa kwenye kinyang’anyiro cha tuzo, ina maanisha amepiga hatua kwewnye kazi zake.

“Tuzo inachangia ofcourse kumtangaza mtu kwenda mbele na kufanikisha kufika mbali, lakini tuzo sio sababu ya kumfanya yeye kufika mbali kwa sababu uliipata baada ya kufika mbali,kinachoanza ni kufika mbali alafu unapata tuzo, kwa hiyo jitihada ndo zinamfanya mtu afike mbali”, alisema Peter Msechu.

Pia Msechu amesema sio kitu kizuri kwa msanii kupata tuzo na kuanza kuona wenzako hawawezi, kwani mpaka msanii anafikia hatua ya kupata tuzo hiyo ni kwa sababu mwengine pia alikuwa kwenye kinyang’anyiro hiko.

“Sio kitu kizuri kama kupata tuzo alafu uone we unaweza wengine hawawezi, kwa sababu mpaka tuseme umepata tuzo ni mwengine amekosa tuzo, ni kwa sababu na yule mwenzako alikuwepo kwenye kinyang’anyiro na wewe ndio ukapata tuzo”, alisema Msechu

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s