Tuzo nyingi haimaanishi unafanya vizuri -Vanessa

Msanii Vanessa Mdee ambaye hivi juzi amechukua Tuzo ya msanii bora wa Afrika Mashariki, amesema kuwa na tuzo nyingi haimaanishi kuwa unafanya vizuri kwenye muziki.

1490702_721529807859749_1396179348_o

Mdee ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio huku akimtolea mfano msanii WizKid ambaye ana tuzo chache lakini muziki wake kufanya vizuri mpaka wasanii wakubwa wanavutiwa kufanya naye kazi.

“Msanii kuwa na Tuzo, kwa mfano tumuangalia WizKid ana tuzo chache, lakini muziki wake unafanya vizuri dunia nzima, Drake anamtafuta, Swizbeat anamtafuta, Alicia Keys ana mtafuta na ratiba yake iko busy mwaka mzima, So haijalishi”, alisema Vanessa ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake wa Never ever.

Pia Vanessa Mdee amewataka wasanii wa muziki wa Bono fleva kuacha kukariri kufanya muziki wanaofanya, kwani muziki umebadilika na watu wanataka muziki mzuri.

“Tuache kukariri, muziki umebadilika kutokana na wasikilizaji, watu wanapenda muziki, masikio yanataka muziki mzuri, kuna wasikilizaji lazima ujichanganye na watu, find watu wanaopenda muziki wako”, alisema Vanessa.

Akiongelea Kolabo yake aliyoifanya na 2Face Idibia kwenye studio za Coke, amesema amefurahi kufanya kazi na msanii huyo mkubwa Afrika, na wasanii wasikate tamaa kwani wana nafasi kubwa ya kufika kimataifa.

“Tulivyokuwa tunashoot nilikuwa na 2face, wengine walikuwa hawajafika, sijawahi kufanya kazi na msanii mkubwa kama yeye, ana heshimu kazi, nimejifunza kitu toka kwake mkarimu, na kuna nafasi kubwa kwa wasanii wa Afrika kufika mbali’, alisema Vanessa.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s