Chameleone atetea msimamo wake

Star wa muziki Jose Chameleone ameutetea msimamo wake wa kushiriki katika wimbo wa ‘Tubonga Naawe’ unaomsifu Rais Museveni pamoja na hafla iliyoandaliwa na kiongozi huyo kwa wasanii mwishoni mwa wiki.

u_4

Chameleone amewataka wote wanaoona hatua hiyo sio sawa, kuacha kushikilia mtazamo hasi na kujua kuwa kila mtu ana msimamo na mawazo binafsi katika kila jambo.

Kwa upande mwingine Eddy Kenzo, msanii mwingine mkubwa Uganda, ametoa mtazamo tofauti kueleza kuwa si busara kwa wasanii waliofanya rekodi ya kumsifu Rais kumuimbia sifa tu, huku kukiwa na changamoto mbalimbali pia chini ya uongozi wake ambazo asilimia kubwa ya watu wangependa kusikia zikigusiwa pia.

Kitendo cha Rais huyo kukutana na wasanii mwishoni mwa wiki na pia kuachiwa kwa rekodi inayomsifu kumeendelea kuzua maoni tofauti kutoka kwa wasanii na Raia, kundi moja likiona ni sawa, huku la pili likiona kuwa wasanii waliofanya hivyo wameangalia maslahi yao binafsi.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s