Jack Chuz Alia Kutopata Mtoto

KARIBU tena msomaji katika kolamu hii inayokuunganisha na mastaa mbalimbali wa muziki na filamu hapa nchini na kupata fursa ya kuwauliza maswali ambayo yamekuwa yakiumiza kichwa huyapatii majibu. Leo tunaye Jack Pentezel ‘Jack Chuz’.

JACKYWACHUZII

Msomaji: Mbali na sanaa unafanya shughuli gani?

Jack Chuz: Nina saluni yangu Sinza na duka la nguo. Pia ni mtaalam wa kusuka na make up.

Msomaji: Nasikia bila ndumba huwezi kukubalika kwenye sanaa, unaliongeleaje hilo?

Jack Chuz: Si kweli, uzuri wa kazi zako ndiyo uchawi wako.

Msomaji: Mumeo (Gadner) ni Muislam na dini inamruhusu wake wanne akitaka kuoa tena utafanyaje?

Jack Chuz: Nitakubali sababu dini inaruhusu ila asije kwa pupa huyo mwanamke tutakosana.

Msomaji: Nilisikia mumeo kakupa talaka tatu, ni kweli?

Jack Chuz: Hakuna kitu kama hicho ni uzushi tu.

Msomaji: Kwa nini mastaa hampendi kuwasaidia chipukizi?

Jack Chuz: Mbona nawasaidia sana tu. Lakini wakati mwingine utakuta mtu anaandaa filamu yake na kuweka chipukizi watupu na hapohapo anahitaji nishiriki katika filamu yake ambayo staa ni mimi peke yangu na hapo nitokee kwenye kava na huwa nafanya hivyo.

Msomaji: Kwa nini kila kukicha unazushiwa ndoa yako kuvunjika na nini siri ya kudumu?

Jack Chuz: Watu wenye chuki ndiyo wanazusha na siri ya kudumu ni maelewano tu, watu wamezoea  kuwa mastaa wengi hawatulii kwenye ndoa.

Msomaji: Tangu umeanza sanaa, umepata mafanikio gani?

Jack Chuz: Kikubwa umaarufu ila kwa maendeleo bado.

Msomaji: Nilisikia hutaki kuzaa na mumeo eti kwa sababu bado unakula ujana na ukipata mimba unatoa?

Jack wa Chuz: Si kweli, natamani kuzaa na mume wangu hata leo. Hakuna kitu kinachoniumiza kila siku kama hicho na kama ipo hospitali inayoweza kunisaidia nitashukuru sana.

Msomaji: Ukikumbuka skendo zako za nyuma unajisikiaje?

Jack Chuz: Huwa naumia sana na kuna kipindi natamani hata nizaliwe upya. Kwa sasa ni Jack mpya kabisa si wa zamani.

Chanzo:GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s