Je Aspirin inazuia kurejea kwa Saratani ?

Utafiti mkubwa na wa kwanza kubaini iwapo umezaji wa tembe za Aspirin kila siku unapunguza kwa kiwango kikubwa athari ya kurejea kwa saratani umeanza.

140806070057_aspirin_tablet_624x351_spl_nocredit

Jaribio hilo linafanyika nchini Uingereza.

Jaribio hilo litahusisha watu 11,000 wanaotibiwa ama waliomaliza matibabu ya aina tofauti za saratani.

Utafiti huu utakaoendelea kwa kipindi cha hadi miaka 12 utatathmini matokeo ya kumeza miligram 300 ya Aspirin kila siku na kutofautisha na kundi lingine litakalokuwa likimeza miligramu 100 ya dawa hiyo.

Makundi hayo mawili yatalinganishwa na kundi la tatu ambalo litakuwa limeza dawa ghushi.

Iwapo utafitu huu utabaini kuwa kweli Aspirin inapunguza athari ya kurejea kwa maambukizi ya saratani basi hii itachochea mwamko mpya katika matibabu ya Saratani ambayo kwa kawaida hugharimu kiasi kikubwa cha pesa.

140821172141_aspirin_624x351_pa

Majaribio hayo yataendeshwa katika vituo 100 nchini Uingereza kwa kipindi cha hadi miaka 12 kuanzia leo.

Onyo hata hivyo limetolewa kuwa Aspirin haifai kutumika na kila mtu bila ya ushauri wa daktari.

Hii ni kwa sababu uchunguzi tofauti ulibaini kuwa umezaji wa dawa hiyo ya Aspirin husababisha vidonda vya tumbo na pia uvujaji wa damu akilini kwa sababu dawa viungo vilivyo kwenye tembe hizo za Aspirin husababisha damu kuwa maji maji.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s