Dumiseheni Amani kabla na baada ya uchaguzi mkuu

Wrriten by Dauka Abraham

Shirika la Global Peace Foundation limewataka Watanzania kudumisha Amani iliyopo katika kuelekea uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika mnamo oktoba 25 mwaka huu na kuweka kando itikadi za vyama vya siasa zilizopo baina yao.

IMG-20151023-WA0001

Akiongea na Habarizao muwakilishi wa shirika hilo Hilda Ngaja ameyasema hayo leo wakati wa mazoezi ya pamoja ambayo yamefanyika Home Gym iliyopo mwenge jijini Dar es salaam yaliyo wakutanisha watu mbalimbali lengo likiwa ni kuwaunganisha wadau tofauti wa siasa nchini.

12185803_1943920102500033_1690561550_o 12186183_1943921815833195_1970325690_o

Ngaja amesema kwasababu siasa sio ugomvi ndiomana wameamua kwaleta pamoja waTanzania katika mazoezi hayo ambayo yameonyesha muitikio mkubwa.

12180952_1943925045832872_1401547429_o 12177313_1943925072499536_922930234_o

“Hawa watu ambao leo wamehuduria katika mazoezi haya ni mabalozi wetu wa kuhubiri Amani kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki zao kwani kati yao wapo wenye itikadi za vyama tofauti lakini pia ni vyema kwa wananchi kukubali matokeo na kutokufanya fujo siku ya uchaguzi,”alisema Ngaja.

12177272_1943925142499529_1043734909_o 11990884_1943920409166669_1327426010_o

Shirika hilo ambalo makao makuu yake yapo katika jiji la Washington nchini Marekani lenye sera ya KURA YANGU AMANI YANGU linashughulika na masuala ya Amani kwa takribani nchi 18 ulimwenguni.

12177076_1943925845832792_1648880145_o 12176127_1943925052499538_806162155_o 12171966_1943925115832865_739392130_o

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s