Q-chief kuwashirikisha Diamond na TID kwenye wimbo wake mpya

Q-chief amemshirikisha TID kwenye wimbo wake mpya ambao bado wapo kwenye mazungumzo na mkali wa ‘Nana’ Diamond ili aikamilishe colabo ya wimbo huo.

qchief6

Akiongea na mtandao wa Bongo5 Q-chief amesema baada ya kumaliza tofauti zake na member mwenza wa kundi lao la zamani la ‘Top Band’ TID ameamua kumshirikisha kwenye wimbo wake mpya ambao tayari TID amesharekodi

“Lakini tumemaliza tofauti zetu, sisi kama watu wazima tunajitambua na nikamwambia hebu tujaribu kufanya ngoma fulani kama aina ya mdumange, ili tujaribu kurudi nyumbani kwa watu wetu. Na ukiangalia wasanii wa kwanza waliofanya vizuri ni Q Chillah na TID.”  Alisema Q

page6

Pia aliongeza kuwa tayari wamemtumia wimbo huo Diamond ili aone anaingiaje

“Kwahiyo tumefanya project kwa Abby Daddy, na Abby Daddy naye yupo kwenye mazungumzo na Diamond ilikuwa aingie kwenye hii ngoma. Tayari TID amemtumia ngoma kwa sababu ametoka kuchukua zile tuzo inabidi tumpongeze halafu tumpe kama wiki moja na nusu then tujue kama ataingia au vipi. Kwa sababu tunajua anaweza kuwa busy sana lakini ile ngoma tayari ni hit. Kwahiyo mwezi wa kumi na moja watu watapata vitu vizuri.” Alisisitiza Q-chief

Source: Bongo5

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s