Uchumba wa Wastara Wavunjika

Uchumba wa mastaa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma na Bond Bin Suleiman ambao ulikuwa umepamba moto huku hivi karibuni ikidaiwa wataoana baada ya uchaguzi, umevunjika baada ya Wastara kusalitiwa.

WASTARA241

Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, wawili hao walikuwa wakienda vizuri lakini hivi karibuni Bond alibainika kumsaliti mwezake kwa kuwa na mwanamke mwingine aliyezaa naye.

“Uchumba wao ulikuwa unaenda vizuri tu lakini mara kwa mara Bond amekuwa akimliza mwenzake kwa kuchepuka. Wastara akawa anaziba masikio kwa kuwa anampenda.

“Kuna wakati Bond alidaiwa kumpa mimba mwanamke aliyefahamika kwa jina la Grace, Wastara akafunika, sasa naona amechoka maana inadaiwa Bond ana mtoto mdogo aliyezaa na mwanamke mwingine.

Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwandishi wetu alimwendea hewani Wastara ambaye alikiri kusikia habari za Bond kuwa na mtoto ila akasema anafuatilia na akijua ukweli atalazimika kujiweka pembeni.

“Mh! Kama hizo habari na nyinyi zimewafikia basi, maana mimi nilizisikia kijuu juu nikaona nitazifanyia kazi ila kiukweli kama ni hivyo, najiweka pembeni. Nimekuwa nikimpigia simu lakini simpati kwa takriban wiki nzima sasa, sijui shida iko wapi,” alisema Wastara.

Chanzo: GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s