Uchumba wa Jack Wolper

ULE uchumba wa mwigizaji Jacqueiline Wolper na Mkongo ambao ulipamba vyombo vya habari kwa miezi kadhaa iliyopita, hatimaye umevunjika rasmi huku daktari wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asili kilichopo Mbezi-Afrikana, Dk. Fadhili Emily akitajwa, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.

wolper872

Wolper alivalishwa pete ya uchumba kwa mbwembwe katika hoteli moja moja maarufu jijini Dar ambapo mwanaume huyo raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo aliahidi kumuoa hivi karibuni huku akijiweka karibu na ndugu wa Wolper.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu na Wolper, kabla Dk. Fadhili hajatia ‘saundi’, tayari Wolper alikuwa ameshapishana na Mkongo huyo hivyo Dk Fadhili alipata kazi rahisi kuvunja uchumba huo maana amekuta unasuasua.

“Wolper alikuwa ameshatofautiana na jamaa, lakini jamaa alikuwa hakubaliani na matokeo akawa anaendeleza uchumba kwa tabutabu sasa alipotokea Dk. Fadhili na kuingiza nyavu, fasta tu Wolper akawa amevunja uchumba wa awali na kuunga uchumba mpya,” alisema mtu huyo wa karibu na Wolper.

Mara baada ya ubuyu huo kutua kwenye dawati la Ijumaa Wikienda, mwanahabari wetu alimtafuta Wolper ili aweze kuzungumzia taarifa hizo ambapo alipopatikana alikiri uchumba wake na kutofafanua vizuri kama uchumba huo umevunjwa na Dk. Fadhili.

“Ndiyo uchumba umevunjika kwani tatizo liko wapi? Kuhusu suala la nani ameuvunjia mbona sioni umuhimu wake, iwe ni huyo dokta (Dk. Fadhili) au mwingine yeyote sawa tu kwani haya si ni maisha yangu binafsi,” alisema Wolper.

Chanzo:GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s