Madai Mazito; Kajala Amharibu Mwanaye!

MSALA! Kuna madai mazito yanayosema kuwa nyota wa filamu Bongo, Kajala Masanja ambaye alizaa na ‘prodyuza’ mkali wa muziki wa kizazi kipya, Paul Matthyssen ‘P Funk’ anamharibu mtoto wao anayefahamika kwa jina la Paula.

PAULA654

Chanzo ambacho pia ni rafiki wa karibu wa familia ya bosi huyo wa Bongo Records, kinasema wazazi hao hivi sasa wako katika mvutano mkubwa kutokana na kinachodaiwa kuwa mabadiliko ya tabia ya binti huyo mwenye umri wa miaka 13, anayesoma kidato cha kwanza katika shule moja iliyopo nje ya Jiji la Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa awali P Funk alikuwa akiishi na bintiye huyo, lakini Kajala hakukubaliana na suala hilo, hivyo akatumia mbinu alizojua na kufanikiwa kumchukua. Kwa ushauri wa marafiki zake, mtayarishaji huyo mtata, aliamua kumuachia mzazi mwenziye amlee, lakini kwa uangalizi wa karibu.

Baadaye, inadaiwa P Funk alianza kubaini mabadiliko kwa mwanaye, ikiwemo kujichanganya na makundi ya wasanii akiwa ameongozana na mama yake, kitu ambacho hakukipenda.

“Wakati anaishi kwa baba yake, Paula alikuwa na uwezo mzuri tu darasani, lakini sasa hivi, anavurunda kutokana na tabia anazofundishwa na mama yake, maana kila mahali alipo Kajala na huyo binti yupo, kwenye vikao na wasanii wa Bongo muvi, wakati mwingine usiku,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta P Funk ili kusikia kauli yake kuhusiana na suala hilo, lakini licha ya kukiri kuwepo kwa tofauti kati yake na mzazi mwenzake juu ya malezi ya mtoto wao, alikataa kuingia kwa undani zaidi, akidai kuwa bize na kazi.

“Yule ni binti yangu, siwezi kuona anaharibikiwa na mimi nikakaa kimya, lazima nikemee, kwa hiyo utofauti upo, lakini kwa sasa sina nafasi ya kulizungumzia hilo,” alisema P- Funk.Risasi Mchanganyiko lilijaribu kuwasiliana na Kajala, lakini juhudi zake hazikuzaa matunda.

Chanzo:GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s