Linah amekana kuwa na ujauzito

Msanii Linah Sanga ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake wa ‘No Stress’ amefunguka na kuweka sawa kuwa hana ujauzito kama ambavyo baadhi ya watu wanavyoongea kwenye mitandao ya kijamii.
Linah

Linah Sanga ameyasema haya kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Television (EATV) na kusema huwa anajipanga ndio maana hajawahi kupata ujauzito pia amedai hana tatizo la uzazi kama baadhi ya watu wanavyohisi.

“Mimi nipo vizuri bhanaa sina tatizo la uzazi ila huwa najipanga ndio maana watu hawajahi kuniona nina ujauzito, lakini kwa sasa najiachia sanaa hivyo muda wowote wanaweza kusikia jambo,” alisema Linah.

Katika hatua nyingine Linah amefunguka kuhusu wasanii kuhusika katika masuala ya siasa amesema wengi wao walikuwa wakifanya kampeni na wameimba sana katika kampeni hizo ingawa suala la kupiga kura lilikuwa ni siri yao wenyewe, hivyo kila msanii kwa nafasi yake ndiye anajua alimchagua kiongozi gani katika uchaguzi mkuu wa 2015 ambao ulifanyika Oktoba 25.

Chanzo: eatv.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s