Arsenal watingwa magoli matano na Bayern

Arsenal wanakabiliwa na kibarua kigumu katika juhudi zao za kutaka kufuzu kwa hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kupokezwa kichapo kikubwa na Bayern Munich.

151104213825_munich_vs_arsenal_512x288_bbc_nocredit

Mambo yalianza kuenda mrama upande wa The Gunners kipindi cha kwanza baada ya bao la kichwa kutoka kwa Robert Lewandowski (dakika ya 10), na makombora kutoka kwa Thomas Muller (Dakika ya 29) na David Alaba (Dakika ya 44)kuwaweka wenyeji 3-0 mbele kufikia muda wa mapumziko.

Arjen Robben kisha alifunga bao dakika ya 55 kipindi cha pili na ingawa Olivier Giroud alifungia Arsenal bao la kufutia machozi dakika ya 69, Muller aliongeza bao jingine dakika ya 89 na kukamilisha kichapo hicho.

Kushindwa huko kwa Arsenal Ulaya, ambako kunafikia rekodi ya kichapo kibaya zaidi kupokezwa timu hiyo barani humo, kinawaacha Arsenal wakiwa alama sita nyuma ya Bayern na Olympiakos zikiwa zimesalia mechi mebili pekee.

Ushindi wa 2-1 wa klabu hiyo ya Ugiriki dhidi ya Dinamo Zagreb unamaanisha kwamba sasa Arsenal hawana usemi kuhusu uwezekano wao wa kufuzu na wamo hatarini ya kushindwa kufika hatua ya muondoano kwa mara ya kwanza katika misimu 13.

Arsenal walikuwa wamepata matumaini majuma mawili yaliyopita walipochapa Bayern 2-0 uwanjani Emirates lakini sasa hayo yote yamefutika.

Sasa lazima wafute pengo la alama sita kati yao na Olympiakos, ambao watakutana nao Desemba 9 baada ya kukutana na Zagreb Novemba 24.

Arsenal wanahitaji kuchapa Zagreb na waombe sana Olympiakos washindwe mechi yao ijayo ugenini kwa Bayern, ambao bado pia hawajafuzu kwa hatua ya muondoano.

Hilo litaacha Arsenal na ‘fainali’ ya kufa kupona nchini Ugiriki ambako Gunners watahitajika kulaza Olympiakos kwa mabao mawili ya wazi, ikizingatiwa kwamba walichapwa 3-2 na klabu hiyo uwanjani Emirates Septemba 29.

Takwimu muhimu

  • Kichapo hicho kinatoshana na kichapo kikubwa zaidi walichowahi kupokeza Arsenal Ulaya, waliposhindwa 4-0 na Milan Februari 2012.
  • Arsenal wamefungwa mabao matano Ulaya kwa mara ya pili sasa (5-2 v Spartak Moscow katika Kombe la Uefa 1982/83).
  • Lewandowski amefunga mabao saba katika mechi zake saba alizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
  • Robben alifunga baada yake kuwa uwanjani sekunde 37 pekee (ilikuwa mara yake ya kwanza kugusa mpira)
  • Giroud amefunga bao katika mechi tatu kati ya nne walizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.

Twaelekea wapi sasa?

Arsenal watakaribisha nyumbani Tottenham Jumapili nao viongozi wa Bundesliga Bayern wawe nyumbani dhidi ya Stuttgart Jumamosi.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s