Taylor Swift ashtakiwa kwa kuiba mistari

Msanii maarufu zaidi duniani kwenye mtandao wa Instagram Taylor Swift ameshtakiwa kwa kuiba mistari ya wimbo wake maarufu Shake It Off.

150622032120_taylor_swift_624x351_getty

Iwapo atapatikana na hati mwanamuziki huyo anakabiliwa na faini ya dola milioni 42.

Mwanamuziki mwenza Jesse Braham vilevile raia wa marekani amedai kupitia kwa wakili wake kuwa Swift aliiba mistari ya wimbo wake alioutunga mwaka wa 2013 unaoitwa ‘Haters Gone Hate’.

Mbali na kufidiwa pesa hizo Braham, anataka jina lake lijumuishwe katika rekodi za wimbo huo kama aliyechangia utunzi wake.

Wakili wa Swift hawajajibu madai ya kesi hiyo inayomkabili.

150624000735_sp_taylor_swift_624x351_pa

Shake It Off uligonga vichwa habari duniani baada ya kutawala chati za muziki wa chapa POP kote duniani.

Umaarufu wa wimbo huo ni wa kupigiwa mfano kwani ni kati ya nyimbo chache zaidi zilizotazamwa zaidi ya mara bilioni moja kwenye mtandao wa Youtube.

Katika Makaratasi aliyowakilisha mahakamani Bwana Braham – ambaye huimba kwa jina ‘Jesse Graham’ – anadai hati miliki ya maneno “haters gone hate” na “playas gone play”, Maneno haya yanatumika kwenye kibwagizo cha wimbo huo wa Taylor.

Kibwagizo cha wimbo wa Braham ni : “Haters gone hater, playas gone play/ Watch out for them fakers, they’ll fake you everyday.”

Kibwagizo cha wimbo wa Taylor Swift ni : “Cause the players gonna play, play, play, play, play/ And the haters gonna hate, hate, hate, hate, hate.”

Katika mstari mwengine Swift anaimba : “And the fakers gonna fake, fake, fake, fake, fake.”

150722172345_taylor_swift_624x351_getty

Kwa mujibu wa mchunguzi wa muziki ,japo maneno hayo yanafanana kimuziki utunzi wa swift haufanani hata kidogo na ule anaodai Brahama.

Braham anasema kuwa amechukua hatua hiyo ya kwenda mahakamani baada ya kujaribu bila mafanikio kutafuta ridhaa kutoka kwa kampuni inayorekodi Swif , Big Machine.

”Nimekwenda kwao mara tatu nne ama hata tano hivi kuwashauri kuhusiana na jambo hilo lakini wamenipuuza.” alisema Braham.

150622051743_taylor_swift_mgm_624x351_getty

Awali anadaiwa kuwa alitaka kupigwa selfi na Swift mbali na kutajwa kama mmoja wa watunzi wa wimbo huo lakini hilo lilikataliwa.

”Lakini kila nilipousikiza wimbo huu,,nafasi yangu iliniandama ,,wimbo huu ni wangu kwanzia mwanzo hadi mwisho”Alisema Braham.

Hii itakuwa kesi ya pili dhidi ya mwanamuziki huyo juma hili.

150323143315_taylor_sweift_624x351_pa

Bwana mmoja DJ huko Marekani David Mueller amemshtaki kwa kudai alimsingizia kuwa alimpapasa.

Mueller anataka fidia kwani anasema siye aliyepapasa Swift bali ni bosi wake.

Alikasirika na kwenda mahakamani baada ya kufutwa kazi na kituo cha redio cha KYGO kilichoko Denver.

Chanzo: bbcswahili

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s