Masanja Kwenye Foleni ya Ubunge Ludewa.. Ataacha Komedi? Asipopita? Viatu vya Marehemu?

Uchaguzi Mkuu Tanzania umekwisha na zile headlines mfululizo kuhusu Siasa zimeanza kupungua pia, lakini hazijaisha… YES !! Bado headlines zitaendelea kutufikia kwa sababu kuna Majimbo ambayo Uchaguzi ulisogezwa mbele baada ya kutokea matatizo mbalimbali ikiwemo Wagombea wake kufariki.

MASANJA32

RIP Marehemu Deo Haule Filikunjombe… stori inagusa Jimbo lake sasahivi, ni Jimbo la Ludewa lililopo Mkoa wa Njombe.

Mchakato kwenye Jimbo hilo umeanza, kwa upande wa CCM ndio kumeshika kasi yenyewe, kwenye majina ya waliotangaza kuitaka nafasi ya Uwakilishi wa Ludewa ndani ya Jengo la Bunge Dodoma, yuko pia mchekeshaji Emmanuel Mgaya a.k.a ‘Masanja Mkandamizaji’ wa Orijino Komedi.

Hii ndio sababu ya yeye kugombea Jimbo la Ludewa Kwanza nina uhakika mimi ndio Mgombea  pekee mwenye uwezo wa kuleta maendeleo… nilikuwa na wazo la kugombea Ubunge lakini  nilijipa muda kwanza– Masanja Mkandamizaji.

Kwanini kagombea kupitia CCM na sio chama kingine  “Mimi ni mwanachama wa CCM na nimeamua kugombea nafasi hii kwa kupitia chama changu, nipo katika siasa tangu siku nyingi ingawa mwanzo sikujitokeza kwa sababu aliyekuwepo alijitosheleza.. nilichukua kadi ya Uanachama wa CCM tangu mwaka 2005.”– Masanja.

Ikitokea hajapita kwenye Ubunge Je?  Nisipopita kugombea Ubunge wa Ludewa, nitampa support yule ambaye  atapewa nafasi kugombea

Orijino Komedi na Ubunge? Hapo vipi mtu wangu ?  Orijino Komedi ipo, mimi sio member wa kundi… mimi ni Mwanzilishi, haimaanishi kwamba nitafanya kazi za Ubunge kwa saa 24 kila siku… maendeleo yatakuja Ludewa lakini Alhamisi kama kawaida, ‘chakachuwa nichakachuweee’… siwezi kuacha Komedi, mbona nilikuwa Mchungaji na sikuacha Komedi.. nitakuwa Mbunge, Komedi na Church…

Wanaojiuliza kama atavaa viatu vya marehemu je?  Naamini ndani ya utawala wangu jimbo la Ludewa litakuwa Jimbo la mfano, kuna wengi wanasema kama nitavaa viatu vya marehemu…! Mimi sijaja kuvaa viatu vya marehemu, ila nitahakikisha maendeleo ya Ludewa yanakua kwa kasi.”-Hivyo ndio alivyomaliza Mchekeshaji anayewakilisha kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji na headlines zake kwenye Ubunge wa Ludewa.

Chanzo: MillardAyo.com

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s