Kombe la dunia lilichangia mimba zaidi Afrika Kusini

Mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, yalichochea ongezeko la idadi ya watoto wa kiume waliozaliwa nchini humo, miezi tisa baada ya mashindano hayo kuanza.

151030145154_nigeria_baby_512x288_bbc_nocredit

Kwa mjibu wa taarifa iliyochapishwa katika jarida la Early Human Development.

Kiwango cha wavulana waliozaliwa katika kipindi hicho kilikuwa kikubwa mno kati ya miaka 2003 na 2014.

Inasemekana kuwa kutokana na mchuano huo wa kombe la dunia wanaume wengi walibaki makwao na hivyo kuchochea kufufuka kwa ndoa zilizokuwa zimefifia.

”watu walikuwa watulivu zaidi, na kuna uwezekano walijihusisha katika tendo la ndoa zaidi wakati wa mashindano hayo ya kombe la dunia, hali iliyofanya ongezeko kubwa ya idadi ya wanawake waliopata ujauzito.” Watafiti wamesema.

Afrika Kusini iliandaa mashindano hayo ya kwanza kabisa barani Afrika kati ya Juni 11 hadi Julai 11 2010.

151107072249_world_cup_2010_fans_624x351_reuters

‘HISIA NZURI’

Dkt Gwinyai Masukume, kutoka Chuo kikuu cha Witwatersrand, alikuwa miongoni mwa waliofanya utafiti huo na akaiambia idhaa ya BBC kuwa

“kombe la dunia liliwafanya watu kutulia mno kiakili, walikuwa na hisia nzuri mno, wakijiwazia mema na pia kufurahia taifa lao.”

“Watu pia walijamiania kupita kiasi wakati wote wa michuano ya kombe la dunia.”

Idadi ya watoto wa kiume waliozaliwa yapata miezi tisa baada ya mashindano ya kombe la dunia ilikuwa asilimia 0.5063, zaidi ya watoto wa kike.

Hii iliashiria watoto wa kiume waliazaliwa takriban 1,088 mwaka uliopfatwa ikilinganishwa na miaka ya awali.

Kisa na maana ”wanaume walishiriki ngono kupita kiasi,kuimarika kwa afya ya manii na kupungua kwa idadi ya watoto wa kiume waliokufa punde baada ya kuzaliwa.

”Kwa hakika haikuwa bahati na sibu”

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s