Aunt: Naapa Wema Ataniona Kwenye Kifo

KIAPO! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwigizaji matata Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Cookie’ kufunguka kuwa kamwe hatajihusisha kwenye ishu yoyote ya sherehe inayomuhusu staa mwenzake Wema Sepetu ‘Madam’ isipokuwa kwenye tatizo la msiba unaomuhusu.

AUNTY37

Kwa mujibu wa chanzo makini, Aunt hakuhudhuria kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Wema, iliyofanyika mwishoni wa wiki iliyopita kwa sababu shosti wake huyo wa zamani hajawahi kwenda kumuona mwanaye tangu azaliwe.

“Aunt hakuweza kwenda kwa sababu bado anachukizwa na kitendo cha Wema kutokwenda kumuona mtoto wake tangu amezaliwa kwa sababu hicho ndiyo kilikuwa kitu muhimu maishani mwake hivyo hata yeye hawezi kwenda kwenye ishu yake yoyote (Wema) ya furaha labda kutokee tatizo la kifo,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Aunt na kuulizwa kama kweli ndiyo wamefikia hatu hiyo na Wema, alikiri kufikia hatua ya kutamka kauli hiyo kwani anashindwa kumuelewa shosti wake huyo ana kitu gani moyoni ambacho kimemfanya ashindwe kumtembelea tangu ajifungue.

“Nashindwa kumuelewa Wema sijui kuna kitu gani kikubwa kinachomfanya ashindwe kumuona mwanangu na sisi tulikuwa marafiki. Siwezi kwenda katika sherehe yake katika hali kama hii tuliyonayo labda kwa ishu ya msiba, nitaennda,” alisema Aunt.Kwa upande wake Wema alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, hakuwa tayari kuzungumzia lolote.

Chanzo: GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a free website or blog at WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: