Mazuu – Wasanii hawana ushirikiano.

Producer Mazuu kutoka Mazuu Records amesema wasanii wa hapa nyumbani hawana ushirikiano na kupeana kazi ambazo zitawatoa kisanii.

033ac90757d2b5d6354d9d02ffc708a9

Mazuu ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, na kueleza kwamba wasanii hufanya hivyo wakihofia kuzidiana kwenye sanaa.

“Kuhusiana na wao wenyewe hawako ‘well organized’, wote wanakuwa kila mtu ana rock kivyake, yani haiwezekani labda mmoja ameona chanell kwamba hii mwenzie ampe ili aweze kufika huko, wasanii wamekuwa hawana ushirikiano, wanakwambia huwezi kumpa mtu siri yako anaweza akakupindua baadae”, alisema Mazuu.

Producer Mazuu aliendelea kwa kusema kuwa kitendo cha wasanii kupinduana pale wanapopata dili nzuri, inatokamna na kuwa na maisha magumu, tofauti na wale wa nje.

“Lakini hii habari ya kupinduana ni kulingana na maisha yamekuwa magumu, mtu anafanya kazi nzuri lakini hafanikiwi, sasa anakuta anapoona mwanya sehemu kama alijiingiza mwenyewe anaona heri akomae yeye ampindue mwenzie ili aweze kufika mbali, tofauti na wenzetu Ulaya, Ulaya muziki umekuwa una chanel, mtu anaona kuna chanel hii hawezi kuifanya kuna mwengine anaweza kuifanya anamualika mwenzio, ila Tanzania hhatuna hilo”, alisema Mazuu.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s