Mimi Siyo Punda Sibebi Madawa–Shilole

Msanii wa kike wa muziki wa Bongofleva Shilole alimaarufu kama ‘Shishi Baby’ amefunguka na kusema habebi dawa ya kulevya kwani yeye si punda ila anapokwenda nje anakwenda kufanya kazi zake na sanaa.

shilole2341

Shilole alipokuwa akipiga stori kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EATV, ambapo amesema watu wengi huwa wanakuwa na dhana hiyo wakidhani labda wasanii wanapokwenda nje huwa wanabeba dawa za kulevya lakini kwa upande wake amekana wazi na kusema anapenda kazi yake ya muziki na kuiheshimu hivyo huwa hafanya kazi hiyo ya kubeba dawa za kulevya.

“Siwezi kukataa ni kweli wapo watu wanakuja kunishawishi lakini namshukuru Mungu nina akili sana hivyo huwa nafikiria sana maisha ya wanangu na kuuweka ushawishi pembeni, na nikimuwaza mpenzi wangu Nuh Mziwanda naona bora hayo mambo yanipite pembeni nisije kuharibu ndoto za maisha yangu na wanangu kwa mambo kama hayo,” alisema Shilole.

Katika hatua nyingine Shilole ameelezea nia yake ya kuja kufunga ndoa na mpenzi wake huyo Nuh Mziwanda na kudai kuwa kwa sasa wanajipanga na muda ukifika watafunga ndoa maana wanataka kufanya harusi kubwa na si kukurupuka tu, kufunga ndoa ya kawaida.

Chanzo: EATV

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s