Ni muhimu kusoma comments za mashabiki – Mr. Blue

Msanii Mr. Blue amesema wao kama wasanii inawawia vigumu sana kujibu maoni ya mashabiki kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii, kutokana na wingi wa maoni hayo.

Mr-Blue1

Mr. Blue ameyasema hayo alipokuwa akiongea na timu ya Planet Bongo ya East Africa Radio, na kueleza kuwa kumjibu mtu mmoja mmoja ni ngumu na itaonyesha upendeleo kwa wale ambao wamepata fursa ya kujibiwa.

“Sio muhimu sana kuwajibu wote kwa sababu utakapo mjibu mmoja na mmoja ukamuacha tayari utakuwa umebagua alafu ni kosa, na ukizingatia wengine wanapata comments zaidi ya elfu tano, kwa hiyo sasa huwezi kujibu comments zote hizo, ina umuhimu kujibu lakini kumjibu mtu mmoja mmoja inakuwa kazi sana, ila tunaweza tukawajibu kwa njia nyingine ya kupost kitu kingine na kuonyesha kuwa umepitia comments zao “, alisema Mr. Blue.

Mr. Blue aliendelea kwa kusema kwamba ni muhimu kwa wao kusoma maoni hayo kwani ni muhimu kwa mashabiki kujua kitu kuhusiana na muziki wao.

“Mi naona wakati mwengine ina umuhimu kwa sababu mashabiki wanataka kujua, labda kuna maswali wanataka kukuuliza ya muhimu ambayo yanahusiana na muziki wako, wanataka kujua either unataka kutoa nyimbo mpya au labda kuna nini kipya kutoka kwako, unaweza ukawajibu isiwe labda kwa mmoja mmoja, lakini ni muhimu kusoma comments”, alisema Blue.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s