Jumuiya ya Ulaya yaipataia Tanzania Milion 464

Jumuiya ya Ulaya (EU) imetiliana saini na mashirika ya umoja wa mataifa yaliyopo nchini Tanzania yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN), wa ruzuku ya Euro 200,000 (sawa na Tsh. 464,000,000) kwa ajili ya shughuli za maendeleo nchini Tanzania.

EU Flag

Akisisitiza mchango wake kwa One UN, balozi wa EU Bw. Filiberto Cerian Sebregondi, amesema kwamba Tanzania imefanikiwa kutengeneza mfumo wa namna bora mashirika ya umoja wa mataifa yanavyoweza kufanya kazi kama taasisi moja katika kuboresha maisha ya watu.

“EU na UN tuna mtazamo mmoja katika masuala ya haki za binadamu, tunu za uhuru, upunguzaji wa umasikini na ulinzi wa mazingira, hata hivyo UN inaamini na kujikita zaidi katika ushirikiano wa kimataifa kama njia ya kukomesha changamoto za dunia zinazogusa amani na usalama, kuondoa umasikini wa kukithiri na mabadiliko ya tabia ya nchi”; alisema Bw. Sebregondi.

Akishukuru nchi za Umoja wa Ulaya, mratibu wa mashirika ya umoja wa mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez amesema kwamba EU imekuwa rafiki na mshirika wa ukweli wa maendeleo wa umoja huo kwa muda mrefu sasa.

“Msaada wa nchi za EU na Eu yenyewe kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa ni muhimu katika kusaidia kufanikisha utendaji wenye ufanisi katika kusaidia maendeleo ya Tanzania, kwa kufanya kazi kwa pamoja katika kushughulikia ajenda, mawasiliano na kuimarisha matokeo ya uangalizi, kutaimarisha mifumo ya ushirikiano ya kimataifa kwa manufaa ya wanaume na wanawake wa Tanzania pamoja na watoto”, alisema Bw. Rodriguez.

Mpaka sasa EU imeshatoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania.

Shughuli hiyo ya utiaji saini imefanyika Ofisi za EU jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa Jumuiya ya Ulaya.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s