Models wetu sio proffesional – Ommy Dimples

Msanii Ommy Dimples amesema sababu ya wasanii kufanya kazi na models wa nje wanapoenda kufanya video ni kutokana na models wa nje kuwa proffesional zaidi kuliko wa hapa nyumbani.

Capture 2_0

Ommy Dimples ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa kuna baadhi ya vitu models wa hapa nyumbani wanashindwa kufanya kutokana na maadili kutoruhusu.

“Mara nyingi models wa nje wako proffesional wanaweza kucheza character zote ambazo wamepangiwa, huku unajua kidogo kuna scene ambazo mtu anatakiwa acheze lets say amevaa swimming costume, unajua huku kumpata msichana ambaye anaamua kujiachia hivyo ni wachache sana, hata kama ikitokea mnaweza mkajikuta msichana huyo huyo atatumika kwenye video za watu wote”, alisema Ommy Dimples.

Ommy Dimples amesema mbali na hayo pia wanafanya hivyo kwa kupunguza gharama za kusafiri na watu wengi, kwani huko wanapatikana kwa urahisi zaidi.

“Kikubwa ni kupunguza gharama, huko wako kibao utawakuta wengi sana, kwa hiyo ndo mana nasema hiyo nayo inachangia, pia ni vigumu kuondoka na watu wote kwenda nao kushoot nao nje, kwa sababu kule unawapata kwa bei rahisi alafu ukilipia video ina maana unalipia kila kitu”, alisema Ommy Dimples.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s