Wasanii Mjipange kwa Magufuli la Sivyo Itakula Kwenu

TANZANIA imepata rais mpya wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli ambaye ameanza kazi rasmi huku Afrika Mashariki ikitegemea mabadiliko makubwa kutoka kwake. Kwenye tasnia ya filamu za Bongo kuna changamoto kubwa na zinazohitaji ufumbuzi makini.

we1

Awamu ya nne chini ya Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alijitahidi kuangazia kila sekta hasa burudani waliokuwa na utaratibu na kujua mahitaji yao sahihi walifaidika kwa kupewa kitu walichohitaji.

Kwa bahati mbaya inawezekana waliofaidika moja kwa moja ikawa ni kwenye michezo zaidi soka kwani waliletewa makocha kadhaa wa kigeni waliochangia kuongeza hamasa ya mchezo huo nchini kuanzia kwenye timu za taifa mpaka katika klabu.

Kwenye filamu, Rais Mstaafu, Kikwete alikuwa na ushirikiano na wasanii mbalimbali kwenye mambo ya kijamii lakini bado kuna changamoto nyingi ambazo awamu yake imeziacha. Inawezekana kabisa wasanii wasipate kiongozi anayeweza kutoa fursa ya kutaka kujua mahitaji yao, tofauti na vile ambavyo wengi wanataka kuongelea matatizo pasipo wao kutengeneza njia sahihi ya kuyatatua badala yake kutumia muda mwingi kulalamika na kunyoosheana vidole.

Sababu za kukosa fursa

Kwenye awamu ya Kikwete, katika filamu pasipokujua kumekuwepo na makundi yanayopingana bila sababu ya msingi, huku wale wanaojiona wana majina wakitofautiana na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF). Inawezekana wazi kuwa, wakati Rais Kikwete alivyoweza kutoa studio kwa wasanii wa muziki na kuleta utata pasipokujua nani anastahili kuimiliki ni wazi ilikuwa ni wasanii kukosa umoja na walioweza kuchangamkia fursa wakafanya hivyo na kuzua mgogoro ulioibukia hadi bungeni.

Hiyo ilikuwa kwa wasanii wa muziki lakini kwa filamu haikuwa hivyo, bado unaona TAFF chini ya rais wake Simon Mwakifwamba wamefanya kazi kubwa katika kuwaunganisha wasanii wengi na kuweza kutafuta fedha kwa wahisani na kufanikisha utengenezwaji wa sera ya filamu lakini bado haijafanyiwa kazi, hii ingetoa dira sahihi katika tasnia ya filamu. Uwepo wa taasisi nyingi zinazojihusisha na filamu bila kuwa na maamuzi ya mwisho nayo ni changamoto kubwa kwani tumeshuhudia vyombo kama Basata, Cosota, Bodi ya Ukaguzi wa filamu na Michezo ya kuigiza sambamba na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) vikilalamikiwa kwa kutolinda maslahi ya wasanii.

Taasisi dhaifu

Mfano ni Baraza la Taifa la Sanaa ndio lililoasisi mashirikisho haya Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (Tafca), Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania (TAPAF) na Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF) lakini mashirikisho haya yaliitisha mkutano na wanahabari kupinga sherehe maalumu ya kuagwa kwa Rais Kikwete. Hili ni tatizo kama kuna vyombo vya kinyonge vikiwa na mamlaka kisheria na havina maamuzi je msanii akihitaji msaada anaweza kupewa? Cosota ni chama cha haki miliki Tanzania, inawezekana ikawa ndio taasisi inaongoza kwa kulalamikiwa baada ya wao kubaki kama chombo cha usululushi huku mtu aliyedhulumu akipewa nafasi kubwa kuliko aliyedhulumiwa kwa kigezo cha uanachama.

Hivi sasa wasanii wengi wa Bongo au watayarishaji chipukizi wanalia kwa kazi zao kuuzwa katika vituo vya televisheni bila idhini yao lakini ukifuatilia utagundua kuwa haramia aliyeuza kwenye runinga husika ana kibali cha Cosota je kutokuwa mwanachama ndio halali kuibiwa?

Nayo Mamlaka ya Mapato (TRA)inalalamikiwa kwa kushindwa kudhibiti wezi wa kazi za filamu pamoja na wasambazaji kununua stempu lakini ndio kwanza wezi wamezidi kuliko awali na hata tasnia ya filamu kuyumba. Bodi ya filamu nayo inalamikiwa kwa kushindwa kushirikiana na TRA kuzuia kazi za kutoka nje zilizojaa nchini.

Chanzo:Mwanaspoti

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s