Irene Uwoya Ashauriwa Aachane na Siasa

Baada ya Irene Uwoya kushindwa kupata nafasi ya vitu maalumu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baadhi ya mashabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV wamemshauri msanii huyo kuachana na masuala ya siasa na kurudi katika tasnia ya filamu.

INENE34

na kuendelea na kazi yake hiyo ya sanaa ambayo imempa jina kubwa na heshima zaidi.

Mashabiki hao wamepokea tofauti taarifa ya kukatwa kwa jina la Irene Uwoya katika katika vitu maalumu, wapo ambao wameonyesha kuguswa na kuumia Irene Uwoya kushindwa ingawa lipo kundi lingine ambalo linaonyesha kufurahia taarifa ya kushindwa kwa msanii huyo ambaye alikuwa moja ya watu ambao walikuwa wakifanya kampeni za uchaguzi kupitia Kundi la Kibajaji.

Yafuatayo ni maoni mbalimbali ya mashabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV kwa Irene Uwoya.

Neema Mgwale: “Hahahaa afadhali kashindwa maana alivyokuwa anashoboka na kuwatukana wasanii wa UKAWA na nilimuona anawaambia wasanii wa UKAWA eti wamemsaliti Jakaya Kikwete kwani alikuwa anawaita Ikulu kila siku yaani hapo ndo nilimwona hafai sababu anathamini kula na rais Ikulu kuliko maisha magumu ya watanzania aendage tuu siasa haimfai”.

Kwa upande wa shabiki mwingine alikuwa na haya ya kusema. “Amshukuru Mungu wake na aamini kuwa kila likuepukalo lina kheri na yeye, kwa sababu CCM inahitaji kubadilisha muelekeo wa bendera yake na kwa sababu hiyo watu wa mzaha mzaha mwaka huu hawana nafasi miaka hii 5 ndio Interview ya CCM kuangalia kama tuwape tena au tusiwape kabisaa na ukumbuke kwenye Interview hatumwi mtoto” ameandika Enock Kayagambe Yahaya.

Chanzo: EATV

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s