Kisa Siasa, Wolper Aweka Pembeni Uigizaji

UPO? Habari ikufikie kuwa ‘mtoto mtamu’ anayesumbua katika tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper Massawe ameweka pembeni masuala ya uigizaji kwa muda usiojulikana kwa kile alichodai ni kujipa muda wa kupumzika na kujikita zaidi kwenye mambo ya siasa.

WOLPER23Rafiki wa karibu na Wolper aliyeomba hifadhi ya jina lake mwanzoni mwa wiki hii, aliliambia gazeti hili kuwa Wolper kwa sasa amekolea sana kwenye mambo ya siasa na kuona kama amekuwa akipoteza muda mwingi kwenye mambo ya uigizaji.

Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, mwandishi wetu alimtafuta Wolper ambaye alikiri kuamua kupumzika kidogo mambo ya uigizaji huku akishindwa kuweka wazi atajikita kwenye nafasi gani ndani ya ulingo wa kisiasa.
“Aah, kila mtu ana mipango na malengo yake, ni kweli kwa sasa nina mambo mengi ya kufanya kupitia siasa, nimejifunza vitu vingi mno vya msingi na muhimu, nimeweka kando kwa muda uigizaji, muda ukifika wa kuendelea na fani hiyo, nitasema,” alisema Wolper.

Chanzo: GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s