Nililazimika kurudi nchini muda ulipoisha – Chege

Msanii Chege toka pande za Temeke amesema alilazimika kurudi Afrika Kusini mara ya pili kwa kuwa muda wa kuwepo nchini humo uliisha na alikuwa hajakamilisha kazi.

Chege ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa radio, na kueleza kuwa baada ya muda kuisha alilazimika kurudi nchini, na kisha kwenda tena kufanya video ya wimbo aliorekodi nchini humo na kumshirikisha msanii Runtown toka Nigeria.

“Nilienda kama miezi miwili nyuma, round ya kwanza nilienda kurekodi audio, muda wa kuwepo kule ukaisha na nilikuwa nimeenda kufanya audio tu, nikaenda tena mara ya pili, wakati tunafanya kazi maporisa alinishauri niweke mnigeria, tukamtafuta Runtown tukafanya kazi, na mpaka sasa nimeshafanya video tayari tunaisubiri kuiachia”” alisema Chege.

Chege amesema pamoja na kuachia video ya wimbo huo aliorekodia nchini Afria Kusini, pia wanatarajia kuachia video ya msanii Temba siku ya tarehe 20 mwezi huu, pamoja na kazi zingine walizozifanya.

Akiongelea kitendo cha Meneja wao Said Fella kuingia kwenye siasa na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Diwani wa kata ya Kirungule, Chege amesema kuwa ingawa anafurahia kitendo hicho, lakni wao kama wasanii wake wataumia kwa kuwa atakuwa na majukumu mengine ya jamii.

“Kwa upande mwingine nimefurahi kwa sababu amekuwa kiongozi, kuna vitu vitakuwa rahisi kwetu na kwake na watu waliomzunguka, lakini kwa upande wa pili kinanisikitisha, najaribu kufikiria mtu akiwa ameingia kwenye uongozi, simu za kina chege na temba zitakuwa hazipokelewi tena, kwa sababu atakuwa busy na majukumu”, alisema Chege.

Chanzo: eatv.tv

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s