Steve Nyerere Alishwa Sumu

STAA wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ hivi karibuni alinusurika kifo baada ya kula chakula chenye sumu na kulazimika kukimbizwa katika Hospitali ya Hurbert Kairuki Memorial iliyopo Mikocheni jijini Dar, Amani  linakupa ripoti kamili.

steve378

Kwa mujibu wa chanzo, Steve alifika hotelini (jina linahifadhiwa) kupata chakula cha jioni na marafiki zake ambapo baada ya kula kidogo akaanza kulalamika tumbo linamuuma.

“Baada ya kula chakula alianza kushika tumbo na kulalamika kwamba alisikia kizunguzungu ndipo wenzake wakambeba na kumkimbika Hospitali ya Kairuki akiwa hajitambui,” kilisema chanzo.

Amani lilipopata taarifa hiyo, lilikwenda katika hospitali aliyolazwa msanii huyo kwa lengo la kujua afya yake ambapo alifungukia tukio hilo kwa masikitiko kwamba  ilikuwa lazima afe.

“Hadi hapa nilipofikia kiukweli namshangaa sana Mungu kwani ilikuwa lazima nife. Nimekimbizwa hospitalini nikiwa sijitambui na nilipochomwa sindano za kitovuni zaidi ya tano, kidogo nikapata ahueni,” alisema Steve.

Steve aliruhusiwa hospitalini hapo juzi (Jumanne) mchana, kwa sasa anaendelea na dozi.

Chanzo: GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s