US yasema ina uhakika kiasi Jihadi John aliuawa

Marekani imesema ina uhakika fulani kwamba mwanamgambo wa Islamic State anayejulikana sana kama Jihadi John, aliyelengwa kwenye shambulio Syria Alhamisi, aliuawa.

151113163210_jihadi_john_512x288_bbc_nocredit

Kanali Steve Warren wa Pentagon alisema shambulio hilo la Alhamisi mjini Raqqa lilipata shabaha, lakini itachukua muda “kutangaza rasmi kwamba shambulio hilo lilifanikiwa”.

Mohammed Emwazi, raia wa Uingereza aliyezaliwa Kuwaiti, alionekana kwenye video akikata shingo mateka kutoka mataifa ya Magharibi.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alisema kumlenga Emwazi lilikuwa “jambo sahihi”.

Inaaminika kwamba kuna mtu mwingine mmoja kwenye gari lililolengwa ambalo lilikuwa limembeba Emwazi, anayejulikana sana kama Jihadi John.

Kanali Warren alisema mashambulio ya mara kwa mara ya Marekani yamekuwa yakiua karibu “kiongoni mmoja mkuu au wa ngazi ya kati wa IS kila siku mbili” tangu mwezi Mei.

Hata hivyo, kifo cha Emwazi kitakuwa “pigo kuu” kwa IS, ingawa hajakuwa akihusika sana katika mipango ya IS au katika uongozi wa kundi hilo.

Kwingineko, maafisa nchini Uturuki wanasema wamemkamata mwanamume raia wa Uingereza, anayeaminika kuwa Aine Lesley Davis, anayedaiwa kuwa mshirika wa Jihadi John. Aine Davis anadaiwa kuwa mmoja wa waliokuwa wakilinda mateka kutoka mataifa ya Magharibi nchini Syria

Chanzo: BBCSWAHILI

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s