Uchaguzi jimbo la Lulindi unafanyika hii leo

Wananchi wa jimbo la Lulindi wilayani Masasi Mkoani Mtwara, leo wanapiga kura katika uchaguzi mdogo wa kumtafuta mbunge wa jimbo hilo, baada ya uchaguzi huo kuahirishwa hapo awali.

Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi – NEC, Dkt Ramadhani Kailima.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt Ramadhani Kailima, imesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kufuatia makosa yaliyofanyika awali katika karatasi za kupigia kura na kupelekea uchaguzi huo kuahirishwa.

Dkt Kailima amesema Tume inasisitiza mambo muhimu mojawapo ikiwa ni pamoja na vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo kuhakikisha vinaweka mawakala wake katika vituo vyote vya kupigia kura na kujumlisha kura. Mawakala hao watatakiwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.

Aidha, mara baada ya kupiga kura na kwa kuzingatia maadili ya uchaguzi ya 2015 yaliyokubaliwa na vyama vyote vya siasa na kuridhiwa na mahakama, wapiga kura wanatakiwa kuondoka vituoni na kuendelea na shughuli zao. Vituoni vyama vya siasa vimeweka mawakala wake ambao watalinda maslahi ya vyama husika na wagombea wao.

Chanzo: eatv.tv

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s