Mimi sina tatizo na Diamond, nampongeza sana sababu tumepata mtu ambaye anatutambulisha kimataifa – Alikiba

Alikiba ametolea ufafanuzi wa Post aliyoiweka Instagram na iliyozua mijadala na hisia tofauti kwa mashabiki wa muziki.

kibaaa-horz

Akiongea na Ala za roho, Alikiba amesema watu wameelewa tofauti post yake na ndio maana ameamua kuifuta

“watu walinielewa vibaya mimi nilikua nawaambia mafans wangu, sababu wao ndo wananipigia Kura mimi sikumaanisha kuhusu tuzo walinielewa vibaya” alisema Kiba.

Pia King kiba alielezea sababu za kutompongeza msanii yoyote aliyeshinda Tuzo hizo japo hata yeye mwenyewe alikua anawania, Kiba amesema kuwa hamna uzalendo

“Siwezi ku-post kitu kuhusu Kushinda Kwao, unajua hakuna uzalendo. watu wangapi wanafanya Vitu vizuri hawapongezwi? Mimi nafanya vingapi? Sisi sio wazalendo…Unajua watu mimi hawanijui Wanahisi kama mimi nina ringa hivi au nina wivu, ila mimi nawapenda wasanii wote pia mziki mzuri” alisema Alikiba.

diamond-afrima

Pia Alikiba alisema kuwa ana tofauti yoyote na Diamond baada ya kuulizwa kuhusiana na uhusiano wao kwasasa

“Mimi sina tatizo na Diamond, nasikia kashida tuzo 3, nampongeza Sana sababu tumepata mtu ambaye anatutambulisha kimataifa ni Kitu poa Sana…Mimi na Diamond we are good” alimaliza Alikiba.

Siku ya Jumatatu Nov.16 Muimbaji huyo wa single mpya ‘Nagharamia’ aliandika, “Asanteni sana najua mmepiga kura sana lakini nilikuja kugundua baada ya kufuatilia kuwa kuna mambo yanaendelea ya watu wanadiriki hata kupoteza pesa zao kwaajili yangu ila nawaomba fans msinielewe vibaya I will always be there for you #hapakazitu #kingkiba,” post ambayo baadae aliifuta.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s