Kassim Majaliwa apita kwa 73.5 % kuwa waziri mkuu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mh. Kassim Majaliwa Mbunge wa jimbo la Ruangwa kuwa Waziri mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

15_0

Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amesoma jina hilo ambalo lilifungwa ndani ya bahasha 3 iliyotoka kwa Rais mbele ya wabunge wa bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Mimi Rais John Pombe Magufuli, kwa mamlaka niliyonayo namteua Ndg. Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, alisikika Spika Ndugai alipokuwa akisoma barua hiyo yenye jina la waziri mkuu.

Kwa mujibu wa katiba Bunge limepitisha uteuzi wa Waziri Mkuu huyo Mhe. Kassim Majaliwa kwa kura 258 za ndio, sawa na asilimia 73.5.

Kassim Majaliwa aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ukuu wa wilaya na naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s