Paris: Aliyepanga mashambulio ameuawa

Mwendesha mashtaka nchini Ufaransa amethibitisha kwamba mwanamume aliyetuhumiwa kupanga mashambulio ya Paris aliuawa kwenye operesheni ya jana.

151118192915_abdelhamid_abaaoud_512x288_ap_nocredit

Abdelhamid Abaaoud ndiye aliyekuwa akisakwa na polisi waliovamia nyumba moja katika mtaa wa Saint Denis, kaskazini mwa Paris jana.

Awali, mwendesha mashtaka wa Paris Francois Molins alikuwa amesema Abaaoud na mshukiwa mwengine Salah Abdeslam hawakuwa miongoni mwa watu wanane waliokamatwa.

Hata hivyo, miili ya watu wawili waliouawa ilikuwa bado haijatambuliwa na baada ya uchunguzi imebainika kwamba Abooud aliuawa.

Hayo yakijiri, wabunge nchini Ufaransa wanatarajiwa kupiga kura kuongeza muda wa kutekelezwa kwa hali ya hatari.

Wapiganaji wa Islamic State (IS), ambao wanadhibiti maeneo ya Syria na Iraq walisema ndio waliohusika katika mashambulio hayo yaliyoua watu 129 na wengine 400 kujeruhiwa Ijumaa.

Gazeti la The Washington Post awali lilikuwa limenukuu maafisa wa Ulaya ambao hawakutajwa majina yao wakisema Abaaoud, 27, aliuawa kwenye operesheni hiyo ya polisi Saint Denis.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s