Steve Nyerere: Nilimwambia Magufuli Kuwasaidia Wasanii wa Filamu ni Kupoteza Pesa

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Club, Steve Nyerere amesema aliulizwa kwa zaidi ya mara sita na Rais Dk John Magufuli kuhusu nsaada wanaouhitaji, lakini amedai alishindwa kumjibu kutokana na wasanii wengi kutojitambua.

STEVE23

Akizungumza katika kipindi cha Take One cha Clouds TV, Steve alisema alimwambia Magufuli asipoteze pesa ya serikali kuwasaidia wasanii wa filamu.

“Sikatai,” alisema Steve. “Nilishamwambia mheshimiwa rais, utapoteza pesa zako, nilisha mwambia mstaafu na huyu mpya utapoteza pesa!

Kwa sababu lazima tukae chini tujitafakari tunataka nini? Mimi ni mtu niliyewahi kuulizwa na mheshimiwa Magufuli zaidi ya mara 6, niliulizwa na mheshimiwa rais tukiwa Morogoro. Serikali haiwezi bila sisi wenyewe kujitambua hata uweke mabilioni ya pesa,” alisisitiza.

Pia Steve alisema wasanii wengi wamejivisha joho la usanii wa filamu lakini hawafanya kazi.

“Kwanza tuna asilimia 90% ya watu kwenye hii industry ya filamu hawajaingia kufanya kazi,” alisema. “Ukichunguza sana watu wamekuja kuuza sura, ukichunguza sana asilimia 90% walioingia kwenye filamu, 6 au 5 ndio wana nia ya kufanya kazi. Hawa wote walioingia wanaingia wapate jina wafanye mambo yao ambayo sio ya kuinua sanaa.”

Kwenye mahojiano hayo pia Steve alisema tasnia ya filamu nchini imefika sehemu mbaya na inaelekea kufa kabisa.

Chanzo: Bongo5

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s