Wanahiphop wa sikuhizi wanazungumzia starehe na pesa tu, Hiphop imepoteza maana – Mwana FA

Msanii wa Bongo Fleva , Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amesema pamoja na kwamba tasnia ya muziki inabadilika, hawezi kuwaunga mkono wasanii wanaopoteza misingi ya muziki wa Hip Hop kwa kivuli cha kutengeneza pesa.

MWANAFA-NEW

“Iko so obvious muziki umebadilika sana, umetoka katika ile misingi iliyowekwa na sababu zake za kuwepo, umekuwa kuhusu starehe na hela peke yake, yani ile misingi imebadilika sana, na vitu vingi ambavyo vilikuwa vinapingwa vilionekana vya kipumbavu mwanzoni huko, sasa hivi ndo kama style, yani vile vitu ambavyo vilikuwa vinapingwa ndio ambavyo watu wanafanya kwa sababu watu wanataka kutrend watengeneze hela” Mwana FA ameiambia Planet Bongo.

FA

Mwana Fa amesema mbali na ukweli kuwa muziki kwasasa umekuwa biashara lakini sio vizuri watu wasio na vipaji kuutumia kuingiza pesa na kuharibu maana ya muziki bora wafanye vitu vingine

“Muziki umekuwa biashara kiukweli, kama unaleta hela why not watu wachukue hela zao, lakini ninachopinga ni kuipoteza kabisa Hip Hop kwa sababu ya hela, kuna vitu vingi vya kufanya na bado ukapata mkate wako wa kila siku, sio lazima usingizie unafanya hii aina ya muziki tunayoifanya wakati huna talent hiyo, sio lazima kujisingizia kufanya kitu ambacho huna uwezo nacho ili tu uingize hela” Alisema Mwana FA.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s