Wema, JB, FA Kuukwaa Ubunge?

NAFASI kumi ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anazo kikatiba kuteua mtu kuwa mbunge, moja itatumika kumteua msanii ili aweze kuwawakilisha wenzake, wanaotajwa zaidi kuukwaa ubunge huo ni Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’, Jacob Steven ‘JB’ na Wema Sepetu.

wema_sepetu31-3

Chanzo cha habari kilicho ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelidokeza gazeti hili kuwa baada ya kushiriki kikamilifu katika kampeni zilizokiwezesha chama hicho kushinda, kimeoni ni jambo la busara kama mmoja wao atateuliwa ili kwenda kuwawakilisha wenzake katika chombo hicho cha kutunga sheria.

“Katika kampeni zake Rais John Magufuli alisema hatawatupa wasanii kwa sababu anafahamu matatizo yao, kwa maana hiyo kuna nafasi kubwa ya mmoja wa wasanii, akateuliwa,” kilisema chanzo hicho huku kikidokeza kuwa majina matatu yanatajwa zaidi kuipata nafasi hiyo.

“MwanaFA yuko vizuri sana kichwani na nadhani anaweza kuwawakilisha wenzake vizuri, Wema ni kwa ajili ya jina lake na JB naye ni mtu anayejitambua, hawa wanatajwa ingawa kama itakubaliwa rais anaweza kumteua mwenyewe,” kilisema chanzo hicho.

MwanaFA alipoulizwa juu ya habari hizo, alisema hana taarifa lakini kama itatokea litakuwa ni jambo la kheri kwani katika hali halisi, wasanii wanahitaji mtu wa moja kwa moja wa kuwawakilisha.

Kwa upande wake, JB alisema hawezi kuzungumzia suala hilo hadi hapo atakapoteuliwa huku Wema Sepetu akishindwa kupokea simu aliyopigiwa.

Gazeti hili lilimtafuta Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye ili azungumzie habari hizo, lakini alipopokea simu na mwandishi kujitambulisha, aliomba atafutwe baadaye kwani kwa muda huo hakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumza. Hadi tunakwenda mitamboni, hakuweza kupatikana tena.

Chanzo: GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s