Hazard akana mvutano na Mourinho

Kiungo wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, amekana madai kuwa uhusiano wake na meneja Jose Mourinho umekumbwa na msukosuko.

150427013322_hazard_640x360_pa_nocredit

Hazard amedokeza kuwa anapania kuendelea kuhudumu Stamford Bridge

Kulingana na Mourinho, Hazard ni miongoni mwa wachezaji ambao wameonyesha matokeo duni sana msimu huu.

Macho yote yamekuwa yakimwangazia Mourinho kufuatia matokeo duni ya mabingwa hao watetezi ambao kwa sasa wanaorodheshwa ya 15 kwenye msimamo wa ligi ya mabingwa huku ikiachwa kwa alama 14 na viongozi Leicester.

“sina tatizo lolote naye. Natumai tutashinda vikombe zaidi pamoja.’

‘Huenda ikawa sio msimu huu kwani ni vigumu sana, lakini misimu ujayo.” Alisema hazard aliye na umri wa miaka 24.

140419073925_eden_hazard_624x351_ap

Blues walitwaa nafasi ya 15 iliyokuwa ikishikiliwa na Norwich baada ya kuitandika 1-0 jumamosi iliyopita.

Ushindi huo ulikuwa ushindi wao wa nne pekee katika mechi 13 walioshiriki msimu huu.

Hazard, ambaye anasemekana yuko njiani kuelekea Real Madrid ya Uhispania hajaifungia Chelsea bao lolote katika mechi 18 .

Hazard alifunga mabao 20 msimu uliopita na kuibuka mshindi wa tuzo za mwanasoka bora wa soka wa kulipwa pamoja na mwanasoka bora wa mwaka katika tuzo ya waandishi wa habari za soka.

Akizungmzia hali yake ya sasa, Hazard alisema,

“sikuanza msimu huu vyema. ‘

”Nilijaribu kujua mbona japo sikujua. Wakati mwingine hujui. Lazime utie bidii.’

‘Nilitia bidii kwenye mazoezi na kwa uwanja nikicheza.

‘Natumai kuregelea hali yangu ya kawaida ili nijaribu kusaidia klabu yangu kushinda mechi”

Chanzo: bbcswahili.com

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s