Hizi ndio kazi ambazo Ney wa mitego andhani Wema sepetu, Adam Mchomvu, Diamond, JB na TID wangefaa zaidi kufanya tofauti na sanaa

Ney wamitego anadhani Wema sepetu, Adam Mchomvu, Diamond, JB na TID wanafit vizuri kwenye kazi zingine tofauti na hizi wanazofanya kwasasa.

Ney wa Mitego ameiambia Millard kazi ambazo anadhani wasanii wenzake wangefaa zaidi kufanya tofauti na hizi za sanaa wanazofanya kwasasa,

Wema Sepetu


Kwa jinsi ninavyomjua Wema nadhani angekua customer care mzuri sana kwenye kampuni yoyote na sauti yake ile angewafurahisha wateja wengi sana. Lakini pia angeweza kuwa mhudumu mzuri tu kwenye hotel flani hivi nzuri nzuri na watu wangeenda kwenye hiyo hotel kwa sababu ya Wema. Anajua kuongea na watu, smile na sauti nzuri.

Adam Mchomvu


Huyu jamaa ana kipaji sana cha kuongea maneno ambayo huwezi kutegemea akaongea ghafla yani yakafurahisha na ku-make sense. Sasa Mchomvu ile kazi ya uswahilini kwetu ya kuuza dawa ya panya,mende,kunguni,viroboto angetisha sana. Hatakua na haja ya kujirekodi sauti na kile ki-speaker atakua anapiga free style tu.

Diamond


Licha ya kufika hapo alipofika Diamond bado uswahili wake wa Tandale anao kama kawaida. Sasa napata picha huyu jamaa awe konda, itakua fujo sana kwenye hilo daladala na abiria wake. Nadhani maneno ya mtaani yatakua mengi na vichambo kama kwenye nyimbo zake..atawanyoosha abiria wake.

JB

 

Huyu jamaa na ule mwili wake ni mpishi mzuri sana zaidi ya kuwa muigizaji alivyo sasa. Pia mapenzi yake kwenye kula msosi basi inaonyesha jinsi gani yeye na msosi ni marafiki kuanzia jikoni hadi mezani.

TID


Huyu jamaa ni muongeaji pia ni mcheshi sana, ukitoa kuwa msanii mzuri basi angeweza kuwa muuza chips mzuri sana maeneo ya kwao Kinondoni na banda lake lingejaa wateja wengi sana kwasababu ya kuongea kwake.

Soource: Millardayo

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s