Kupa Apigwa Chupa Klabu

MSANII wa filamu za Kibongo, Rashid Makupa ‘Kupa’ hivi karibuni alikuwa katika wakati mgumu baada ya kupigwa chupa kichwani na Kundi la Panya Road lililovamia sherehe ya kuzaliwa ya msanii mwenzake, Maira Mlope.

kupa3

Tukio hilo lilitokea ndani ya Klabu ya Philemon Lounge, Kinondoni-Manyanya jijini Dar ambapo lilizuka varangati baada ya kijana mmoja aliyekolea ulabu kutoka nje ya klabu hiyo na kulichokoza kundi hilo lililokuwa likipita na kulazimika kuingia ndani likiwa na silaha mbalimbali kama vile visu, bisibisi na marungu na kumkuta Kupa aliyekuwa mshereheshaji (MC).

Baada ya kuingia, Panya Road walizua bonge la timbwili ukumbini humo na kuvurumisha chupa ovyo ambapo Kupa alijeruhiwa kichwani na alipopata upenyo akakimbia.

Kona ya Bongo Movies ilimuhoji Kupa kufuatia tukio hilo ambapo alisema:
“Ohooo…kaka hapa siyo, hali ishachafuka ngoja tusepe, hebu nicheki hapa kichwani nimepigwa chupa nasikia maumivu makali sana.”

Chanzo: GPL

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s