Sijapenda majibu ya Harmonize – Rose Ndauka

Msanii Rose Ndauka amesema kitendo cha msanii Harmonize kujibu majibu yenye utata alipokuwa akihojiwa na kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Televisio, hakupendezwa nacho kwani kinazidi kuleta sintofahamu.

Rose Ndauka ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba Harmonize alitakiwa kujibu moja kwamoja kuwa hawana mahusiano yoyote zaidi ya kufahamiana nae kikazi.

“Mi Harmonize namfahamu kama msanii, na hii issue sio mara ya kwanza, tayari nilishaona alihojiwa kwenye interview nyingine alihojiwa kuhusu mimi, what I didn’t like ni kwamba angeongea straight, unajua kama huna mahusiano na mtu na ukaulizwa unaongea moja kwa moja, kitendo cha kutengeneza mazingira na watu wakaanza kuweka doubt kwamba Rose na Harmonize watakuwa na mahusiano, hicho ni kitu ambacho mimi sikukipenda”, alisema Rose Ndauka.

Rose Ndauka aliendelea kwa kusema kwamba yeye na Haronize hawana mahusiano kama ambavyo Harmonize alielezea, na kwamba iko tofauti na watu wanavyofikiria.

“The way alivyolijibu ilo suala kwamba mimi na yeye tunafahamiana kwamba naongea nae sana, mi na Harmonize hatuongei sana, na hata kama tunaongea labda Rose naomba nipostie hiki, sio kwamba ni mtu ambaye namfahamu sana au tuna mahusiano ya karibu sana, iko tofauti sana na yeye alivyojibu”, alisema Rose Ndauka.

Wiki iliyopita Harmonize alihojiwa kuhusu uhusiano wake na Rose Naduka kwenye kipindi cha Planet Bongo baada ya kuonekana wana ukaribu sana, na kutoa majibu ambayo yalileta sintofahamu kwa jamii.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s