Mwili wa marehemu Mawazo kuzikwa kesho

Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita Alphonce Mawazo umeagwa leo Geita Mjini na unataraji kuzikwa kesho Katika kijiji cha Chikobe mkoani Geita.

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita Alphonce Mawazo umeagwa leo Geita Mjini na mamia ya wananchi wakiongozwa na mweyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe.

Shughuli hiyo ya kuuaga mwili huo mkoani Geita pia ilihudhuriwa na aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye pamoja na wabunge 50 wa CHADEMA.

Mwili wa Mawazo umeagwa pia katika jimbo alilogombea ubunge la Busanda ambapo ulipokelewa na mamia ya wananchi ambao walilibeba jeneza lake kwa umbali wa zaidi ya kilomita moja hadi katika uwanja wa Mnadani CCM ambapo ndipo shughuli za kuuga zimefanyika.

Marehemu Alphonce Mawazo aliyeuwawa kwa kukatwa na mapanga Novemba 14, katika kijiji cha Katoro na watu wasiojulikana atazikwa kesho kijijini kwao Chikobe tarafa ya Butundwa Mkoani Geita.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s