Alex wa Ghetto Kids afariki dunia kwa ajali.

Mtoto Alex ambaye ni mmoja wa watoto wanaounda kundi la Ghetto Kids ambao wanafanya kazi na msanii toka Uganda Eddy Kenzo amefariki dunia, na mwengine ambaye anajulikana kwa jina la Patricia yuko katika hali mbaya, baada ya kupata ajali ya baiskeli.

Kwa Mujibu wa Willyam Marshal ambaye ni mmoja wa watu wao wa karibu amesema wawili hao walikuwa wakiendesha baiskeli, ambayo ilikatika breki na kutumbukia kwenye mtaro, na kujigonga kwenye mawe na kupelekea Alex kuvunjika shingo, na kuwakakimbizwa kwenye hospitali ya Nsambya ambapo baadaye wakamuhamishia hospitali ya Rubaga, na kufariki dunia akiwa njiani.

Msanii Eddy Kenzo amempeleka Patricia ambaye yupo kwenye hali mbaya kwenye hospitali binafsi kwa ajili ya matibabu mazuri, na madaktari wamesema anaendelea vizuri ingawa bado yupo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

Pia msanii Eddy Kenzo amewataka watu kumuombea Patricia wakati huu ambao anaendelea kupata matibabu na kuandika haya kwenye ukurasa wake wa twitter na facebook, na kumuombea Alex apumzike kwa amani.

“Doctors said Patricia will be fine.But is she is still in intensive care let’s keep playing, Alex has gone to be with the Lord, he passed on this evening in an accident, he featured in Sitya Loss and so good videos. Rest in eternal peace young soldier”, alisema Eddy Kenzo.

Alex na Patricia walikuwa ni miongoni mwa watoto waliounda kundi la Ghetto Kids ambao walijipatia umaarufu duniani baada ya kucheza video ya wimbo wa Sitya loss wa Eddy kenzo na kuwa miongoni mwa video zilizotazamwa kwa wingi ulimwenguni.

Patricia wa Ghetto Kids ambaye yuko mahututi.
Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s