Sipendi kushindanishwa na Vanessa Mdee – Shaa

Msanii Shaa ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa ‘Toba’ amefunguka na kusema hapendi kushindanishwa na msaniii Vanessa Mdee.

Shaa wakati akipiga stori kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EATV ameonesha wazi kukerwa na kutofurahishwa na kitendo cha baadhi ya mashabiki kuanza kuwapambanisha na kuwafananisha kisanii wasanii wa nyumbani.

“Niwambie ukweli sipendi sana hii tabia ya watanzania kunishindanisha na Vanessa Mdee au kitendo cha kuwashindanisha wasanii wa nyumbani, huwezi kuwashindanisha watu ambao wapo kwenye boti moja, Mimi Shaa pamoja na Vanessa Mdee wote tunapeperusha bendera moja ya Tanzania hivyo unapotupambanisha ili iwe nini ni bora hata ungenipambanisha na msanii kama Yemialadee sababu yule ni msanii kutoka nchi nyingine” Alisema Shaa

Mbali na hilo msanii huyo amesema wimbo wake ‘Sugua Gaga’ ni wimbo ambao umemuingizia pesa nyingi zaidi ya nyimbo zingine za zamani na wimbo huo umemuwezesha kufanya video nyingine tatu, Shaa amesisitiza wimbo wa Toba uliandikwa na msaniii H Mbizo na hakubadilisha kitu hata kimoja.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s