Naona napoelekea-Belle9

Msaniii Belle 9 ambaye anauwakilisha vyema mkoa wa Morogoro na viunga vyake katika muziki amefunguka na kusema kwa sasa anaona anapoelekea kimuziki na kuona mafanikio ya kazi zake hizo.

Akipiga stori kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio msanii huyo amesema toka amekuwa chini ya uongozi wa Vitamin Music amenza kuona anapoelekea kimuziki pamoja na maisha ya kawaida, kwani amepata wigo mpana wa kufanya kazi chini ya usimamizi na kuweza kufika mbali zaidi.

Meneja wa Belle 9 aliweka wazi kuwa haikuwa kazi ndogo kumbadili msanii huyo mpaka kufikia sasa hatua aliyonayo sasa lakini walikuwa wakiaamini kuwa angeweza sababu anakipaji na uwezo huo, katika hatua nyingine meneja huyo aliweka wazi na kumtambulisha Dj Summer wa East Africa Radio kuwa ndiye Dj rasmi wa Belle 9 kwa sasa.

Mbali na hilo Belle 9 jana ametambulisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Bugger Movie Selfie ambao umeandaliwa na producer kutoka Morogoro, lakini hata video ya wimbo huo imefanyika Morogoro chini ya director kutoka mkoa huo wa Morogoro.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s