Atemwa Yanga, asaini miaka miwili Korea

KIUNGO wa pembeni, Mbrazili, Andrey Coutinho, aliyesitishiwa mkataba na Klabu ya Yanga, mwanzoni mwa wiki hii, tayari amepata dili la kusaini miaka miwili kuitumikia Kwampong inayoshiriki Ligi Kuu ya Korea.

TINYO

Inajulikana kuwa chanzo kikubwa cha kuondoka kwa mchezaji huyo klabuni hapo ni kutokana na kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo kilichopo chini ya Kocha Mholanzi, Hans van Der Pluijm lakini Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amefafanua kilichokuwa nyuma ya pazia.

Tiboroha ameliambia Championi Ijumaa kuwa Coutinho ameuzwa akiwa kama mchezaji huru ambavyo ni tofauti na watu walivyokuwa wakifikiria lakini pia amekanusha taarifa za kwamba wao ndiyo waliomtema mchezaji huyo na badala yake ni kwamba Coutinho alitaka kuondoka mwenyewe.

“Coutinho amepata dili la kucheza miaka miwili huko Korea kwenye timu ya Kwampong. Coutinho ameondoka akiwa kama mchezaji huru baada ya kumalizana naye katika mkataba wake uliobaki, kuhusu tulilipana au ilikuwaje, hiyo inabaki kuwa siri yetu lakini ndivyo ilivyokuwa.

“Unajua ningependa watu waelewe kwamba Coutinho si kwamba tulimuondoa, ni kwamba aliomba kuondoka yeye mwenyewe na ishu ilikuwa ni kutopata nafasi, kwa hiyo tukamalizana naye na sasa yupo Korea,” alisema Tiboroha.
Kuondoka kwa Coutinho kikosini hapo, kumetoa nafasi ya Yanga kuvuta mchezaji mpya wa kimataifa, Mniger, Issofou Boubacar kumfanyia majaribio na kama akifuzu, basi watamsajili.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s