Shehena la vipodozi lakamatwa Morogoro

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata shehena ya vipodozi vinavyodaiwa kuwa ni bandia na vilivyo ingizwa nchini kinyume na sheria ambapo watu watatu wanashiliwa na jeshi hilo kutokana na tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonald Paulo

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonald Paulo amesema shehena hiyo ya vipodozi imekamatwa eneo la modeco mjini Morogoro ikiwa inashushwa kutoka kwenye lori tupu la mafuta ya petrol,lililokuwa likitoka Zambia kupitia mpaka wa Tunduma, aina ya track tanker namba t 927 CHX, na Tela namba T692 CJE.

Vipodozi vilivyokamatwa ni pamoja na Betasal,Diproson,Citro Light na Top Lemon ambapo kamanda huyo wa polisi ameahidi kushirikiana na mamlaka ya mapato nchini TRA,na TFDA, sambamba na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa tukio hilo.

Jumamosi mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kati wameteketeza shehena ya madawa na vipodozi bandia,vyenye kemikali za sumu na vilivyoingia nchini kinyume na sheria katika wilaya ya Kilosa baada ya msako mkali kwenye maeneo ya ruaha,kilosa na mikumi na kuwaonya wananchi kuacha kutumia bidhaa hizo,huku wakiwaonya pia wafanyabiashara wanaoingiza kinyemela bidhaa hizo.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s