Samatta katika orodha ya 3 bora ya CAF

Mshambulizi matata wa Taifa Stars ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mbwana Samatta ametajwa katika orodha ya wachezaji watatu bora na shirikisho la soka la Afrika CAF wanaocheza soka barani Afrika.

Samatta anawania hiyo na wachezaji wengine wawili Baghdad Boundjah wa Algeria na Etoile du Sahel na Kipa machachari wa TP Mazembe ya DR Congo Robert Kidiaba.

Mshindi atachaguliwa na makocha wa timu za taifa na kutangazwa katika dhifa maalum Januari tarehe 7 mwakani.

CAF ilikuwa imewataja wachezaji 37 katika orodha ya awali lakini wakachuja hadi 10 mwezi uliopita.

 

Siku chache tu baada ya kutawazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na shirika la BBC Yaya Toure, ametajwa miongoni mwa wachezaji watatu bora kuwania taji la mwanakandanda bora mwaka huu na Shirikisho la soka barani Afrika (Caf).

Tuzo hii huwajumuisha wachezaji wa Afrika wanaocheza soka ng’ambo.

Nyota huyo wa Manchester City kwa mara nyengine atakuwa akipigania taji hilo dhidi ya mshambulizi wa Black Stars ya Ghana na Swansea Andre ‘Dede’ Ayew na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund.

 

Endapo atashinda kigogo huyo wa The Elephants ya Ivory Coast Yaya Toure, atakuwa mtu wa kwanza kunyakua taji hilo kwa mara ya tano.

Toure, ambaye aliiongoza Ivory Coast kutwaa ubingwa wa mataifa ya Afrika mapema mwaka huu pamoja na aliyekuwa nahodha wa Cameroon Samuel Eto’o ndio wachezaji wa pekee waliowahi kutwaa taji la mchezaji bora wa Afrika mara 4.

Eto’o alitwaa taji hilo katika miaka ya 2003, 2004, 2005 na 2010.

Wanaowania tuzo za 2015 ya CAF

Mchezaji bora mwanamke 2015:

 • Gabrielle Onguéné – Cameroon
 • Gaelle Enganamouit – Cameroon
 • Ngozi Ebere – Nigeria
 • N’rehy Tia Ines – Ivory Coast
 • Portia Boakye – Ghana

Chipukizi bora wa 2015:

 • Adama Traore – Mali
 • Kelechi Nwakali – Nigeria
 • Samuel Diarra – Mali
 • Victor Osimhen – Nigeria
 • Yaw Yeboah – Ghana

Anayeonesha matumaini:

 • Azubuike Okechukwu – Nigeria
 • Etebo Oghenekaro – Nigeria
 • Djigui Diarra – Mali
 • Mahmoud ‘Kahraba’ Abdelmonem – Misri
 • Zinedine Ferhat – Algeria

Kocha bora mwaka 2015:

 • Baye Ba – Mali U -17
 • Emmanuel Amunike – Nigeria U -17
 • Fawzi Benzarti – Etoile du Sahel
 • Hervé Renard – Ivory Coast
 • Patrice Carteron – TP Mazembe

Refarii bora mwaka 2015:

 • Alioum Neant – Cameroon
 • Bakary Papa Gassama – The Gambia
 • Eric Arnaud Otogo Castane – Gabon
 • Ghead Zaglol Grisha – Egypt
 • Janny Sikazwe – Zambia

Mwafrika aliyebobea:

 • CK Gyamfi – Ghana
 • Samuel Mbappé Léppé – Cameroon

Timu bora ya taifa :

 • Ivory Coast
 • Ghana
 • Mali U-17
 • Nigeria U-17
 • Nigeria U-23

Timu bora ya taifa ya wanawake:

 • Ghana,
 • Cameroon,
 • Afrika Kusini,
 • Zimbabwe

Klabu bora 2015:

 • USM Algers – Algeria
 • TP Mazembe – DR Congo
 • Orlando Pirates – Afrika Kusini
 • Etoile du Sahel – Tunisia
Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s