Hermy B amejipanga atabadilisha muziki wa Tz- AY

Mwanamuziki mkongwe wa bongo fleva Ambwene Yesaya (AY) amefunguka na kusema mtayarishaji na mmiliki wa studio ya B’Hits Music Group , Hermy B atabadili aina ya muziki ambao upo Tanzania kwa sasa

Akipiga stori katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa na kituo bora cha vijana nchini (EATV) AY alidai kuwa kipindi ambacho hawakuwa sawa na mtayarishaji huyo ni kipindi alichokitumia kujijenga zaidi na kuja na sound mpya katika muziki wa bongo fleva ambayo yeye AY anaona italeta mabadiliko kimuziki.

” Tunashukuru matatizo yetu tulitatua ila katika kipindi hicho unaona kabisaa Hermy B alikuwa anajipanga na sisi pia tulikuwa tunajipanga, saa hizi ana sound mpya kabisa naamini itabadili aina ya muziki ambao upo nyumbani na kwa kuanza itatoka kazi ya ‘Mwana FA” na kuna kazi zangu zitakuja pia ameshafanya kazi na Fid Q na wasanii wengine ” Alisema AY

Mbali na hilo AY alizungumzia kufurahishwa na ushirikiano uliopo katika muziki kwa sasa hususani kwa maproducer na kusema ni jambo jema kwani producer huyu anaweza kufanya jambo fulani na kazi hiyo ukaenda nayo kwa producer mwingine akaongeza jambo jingine kwa lengo la kuboresha kazi iwe bora zaidi.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s